u/Shot-Poetry5724

Not a Job Post, Looking for a Real Technical Co-Founder to Build a Trust & Fraud Intelligence System for Mobile Transactions in Tanzania
▲ 9 r/tanzaniatechnology+1 crossposts

Not a Job Post, Looking for a Real Technical Co-Founder to Build a Trust & Fraud Intelligence System for Mobile Transactions in Tanzania

I’m currently exploring a long-term technical co-founder relationship for an early-stage system called ChekiNamba.

Problem yenyewe ipo around trust & fraud kwenye phone-number based transactions, especially kwenye mobile money ecosystem ya Tanzania.

Simple idea ni hii:

Unawezaje kujua kama number ina trust before kutuma hela?

Hii sio corporate hiring wala normal job post.

Natafuta watu ambao:

- wanapenda systems thinking

- wanaelewa security/adversarial thinking

- wanapenda kujenga real systems

- wako comfortable kufanya vitu kwenye uncertainty

- na ideally washawahi build projects before

Current stage:

- bado early-stage

- product scope bado tunaiexplore

- hakuna massive funding bado

- more of founder-level collaboration

Interested sana na watu wa:

- Computer Science

- Software Engineering

- Information Systems

- Cybersecurity

- backend/API systems

- au hata self-taught builders wenye real projects

Kwa sasa priority ipo zaidi kwa watu wa Dar kutokana na ease ya collaboration kwenye hatua hii ya mwanzo.

Nimeamua kutumia structured form instead ya random DMs ili iwe easier kupata watu wenye strong thinking & serious mindset.

Applications zitareviewiwa selectively na form inaweza kufungwa mapema tukipata watu strong.

Application form : click here

Kama una deeper thoughts/questions unaweza pia kutuma kupitia:

info@chekinamba.com.

u/Shot-Poetry5724 — 3 days ago
▲ 38 r/tanzaniatechnology+1 crossposts

Habari wakuu!

​Sote tunajua kero ya utapeli unaofanyika kwa njia ya simu. Iwe ni meseji za "Tuma pesa kwenye namba hii", watu wanaojifanya ni huduma kwa wateja wa mitandao (Vodacom, Tigo, Airtel, Halotel), au matapeli wa bidhaa mitandaoni (Instagram/Facebook). Lengo letu ni moja: Kuhakikisha namba ya tapeli yeyote yule haipumui.

​Nimeamua kutumia utaalamu wangu wa Tech kutengeneza Cheki Namba—jukwaa linalounganisha jamii kupambana na aina zote za uhalifu unaofanyika kwa njia ya simu nchini Tanzania.

​Inafanyaje Kazi?

​Ni rahisi: Kabla ya kutuma pesa au kutoa taarifa zako, ingia kwenye mfumo na uhakiki namba hiyo.

​Hali ya sasa: Kama namba imeripotiwa kama ya kitapeli, mfumo unakuonya papo hapo 🚩.

​Wajibu wako: Kama umekutana na aina yoyote ya utapeli kwa njia ya simu, iripoti (Submit Report) namba hiyo ikiwa na ushahidi. Kila namba unayoiripoti inakuwa 'Blacklisted' na kumlinda Mtanzania mwingine asitapeliwe kesho.

​Tulipofikia (New Updates):

​Kariakoo Pilot Phase: Tumeshaingia mtaani! Tumeshaanza majaribio na wafanyabiashara wa Kariakoo kuhakikisha mfumo unalinda miamala ya kweli ya biashara.

​PWA Technology: Huna haja ya kudownload App. I-install moja kwa moja kwenye browser yako (Add to Home Screen). Ni nyepesi, salama, na haili storage.

​Data Integrity: Tunatumia IP tracking & Rate limiting kuzuia ripoti za uongo. Tunataka database yenye ukweli 100%.

​Sheria, Faragha na Ulinzi wa Mtumiaji:

​Tumejipanga kisheria na kiufundi kulinda jamii:

​Privacy Policy & Terms of Service: Tunazingatia Sheria ya Ulindaji wa Taarifa Binafsi (2022). Tunakusanya IP kwa ajili ya usalama wa mfumo tu kuzuia Spam.

​Disclaimer: Cheki Namba ni chombo cha kutoa tahadhari (Advisory tool). Maamuzi ya mwisho ya kifedha yanabaki kwa mtumiaji.

​Request Removal: Tunaruhusu ombi la kuondoa namba kama kuna namba imeripotiwa kimakosa baada ya uhakiki wa kina.

​Msaada wa Kisheria: Tunakaribisha mwongozo na msaada wa kisheria kutoka kwa wadau wa PDPC na TCRA ili kuhakikisha mfumo huu unakua ndani ya misingi ya sheria za nchi.

​Roadmap Yetu:

​WhatsApp Bot & USSD: Kwa ajili ya urahisi wa chati na watumiaji wa "vitochi".

​API for Banks & Telcos: Maono yetu ni kuunganisha database hii na mitandao ya simu na mabenki ili kuzuia muamala wa kitapeli kabla haujakamilika.

​Database bado inakua kila siku, na nguvu ya mfumo huu ipo mikononi mwetu. Kama kuna aina yoyote ya tapeli aliyewahi kufanya uhalifu kwa njia ya simu, namba yake inatakiwa iishie hapa Cheki Namba.

​Icheki hapa kuangalia Terms zetu

​Tujilinde, tujenge jamii yenye uaminifu. 👊

u/Shot-Poetry5724 — 15 days ago
▲ 27 r/tanzaniatechnology+4 crossposts

Habari zenu wakuu!

Kama kijana wa Kitanzania na tech enthusiast (UDSM student), nimechoshwa na kila siku kusikia ndugu, rafiki, au wazazi wetu wameibiwa pesa zao na hawa matapeli wa simu. Ile michezo ya "Nitumie kwenye namba hii" au "Nitumie ada ya kutolea" imekuwa kero ya kitaifa inayorudisha nyuma Financial Inclusion.

Nimeamua kutumia muda wangu wa ziada kucode suluhisho linaloitwa Cheki Namba.

Cheki Namba ni nini?

Ni "Trust Layer" huru kwa ajili ya miamala ya simu. Badala ya kutegemea mtoa huduma mmoja, tunatumia nguvu ya jamii (Crowdsourcing) kutambua walaghai mapema.

Key Features I’ve Integrated:

  1. Search & Verify: Mtumiaji anaweza kuhakiki namba na kupata majibu ya papo hapo (Safe/Caution/Danger) kulingana na data iliyopo.
  2. Crowdsourced Reporting: Wananchi wanaweza kuripoti namba, aina ya utapeli (scam type), na kutoa maelezo ya tukio.
  3. AI Moderation (In Development): Tunatumia AI kuzuia "false reporting" na "spamming". Mfumo haumpiki mtu kuwa tapeli kwa ripoti moja tu; tunatumia Reputation Scoring na Cross-validation kabla ya kutoa "Red Flag". (To be integrated)

Technical Stack & Compliance:

  • Backend: Node.js/Python (Railway hosted for high availability).
  • Data Privacy: Hili ni eneo nyeti. Tayari nimeanza mchakato wa usajili na PDPC (Personal Data Protection Commission) kama Data Controller kufuata sheria ya 2022. Tunakusanya data muhimu tu kwa ajili ya usalama na tuna "Data Removal Request" policy.
  • Scalability: Mapema mwezi wa tano nimepanga kuongeza WhatsApp Bot na USSD (via aggregators) ili kuwafikia watu wenye simu ndogo (vitochi) ambao ndio wahanga wakuu.

The Roadmap (Startup Vision):

Lengo langu siyo kuishia kwenye website tu. Natafuta kuijenga Cheki Namba kuwa API service ambayo mabenki (kama CRDB/NMB) na MNOs wanaweza ku-integrate kwenye Apps zao kuzuia fraud kabla hata ya transaction kukamilika.

Naomba msaada wenu (The Ask):

Hii bado ni MVP .Naomba mui-test hapa:

👉 https://chekinamba-production.up.railway.app

Nipe maoni yako ya kitalamu:

  1. Security: Unadhani kuna "loopholes" gani naweza kuziba kwenye upande wa data?
  2. Ethics: Je, unaona kuna hatari ya watu kusingiziana (defamation), na nini kiongezwe kudhibiti hilo zaidi ya AI moderation?
  3. UI/UX: Je, interface ni rahisi kutosha kwa mtu asiye wa tech?

Pesa yetu ni jasho letu, tusiwaachie hawa wahuni kirahisi. Nipo hapa kujibu maswali yote na kupokea "constructive criticism".

Asanteni sana! 🛡️✊

u/Shot-Poetry5724 — 16 days ago