Miamala kukwama hewani, aghh!
Aisee... hii mitandao ya TZ imenishinda kabisa, nimeshatumia Vodacom, TIGO (YAS), Airtel, Halotel, TTCL... hakuna mtandao hata mmoja wenye uafadhali.
Nina laini 7 za mitandao 5 tofauti, kila laini ina kazi yake na hii ni kutokana na huduma mbovu zilizopo TZ kwenye mitandao ya simu.
Nimeandika huu uzi baada ya YAS kufeli kukamilisha muamala wa kwenda Selcom na hapo ni baada ya Mastercard yao kushindwa kufanya muamala online, nikaamua niipeleke pesa Selcom ili nitumie virtual card yao matokeo yake pesa yangu imebaki hewani na mteja ndiyo naangushiwa hasara kwa muda wote pesa yangu inapokuwa hewani.
Juzi TTCL nao walinifanyia michezo hii-hii, pesa ilikaa hewani siku 4, mara ya kwanza kutoa taarifa huduma nikaambiwa nisuburi masaa 24, simu zilizofuata ni dana-dana tu "subiri masaa machache" mpaka masaa 96 yakapita pesa yangu wanayo wao tu, kirahisi-rahisi tu wao hawapotezi chochote. 🤬
Bongo miyeyusho sana, inapaswa hii mitandao iwe inatoa taarifa kila mteja anapofaya muamala kama mifumo haisomani kwa wakati huo ni bora mtu asitishe huo muamala... hii tabia pesa wanakata halafu wanakaa nayo kama ya kwao inaumiza sana hasa kama ni pesa ya dharula!